Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, wafanyakazi wa Google waliandamana kutokana na ushirikiano wa kampuni hiyo na Israel katika mauaji yanayoendelea huko Ghaza, na walisisitiza kuwa endapo hatua hizo zitaendelea, basi watafanya mgomo.
Watatu kati ya wafanyakazi wa Google, katika mahojiano na gazeti la "Financial Times", walisema: "Kilichowasukuma wafanyakazi kufikia hatua hii ni ripoti za vyombo vya habari kuhusu matumizi ya Israel ya "akili mnemba" kwa kushirikiana na Google, kwa ajili ya kulenga Ghaza na kuwaua watu wa eneo hilo.
Kadhalika, baadhi ya waandaaji wa maandamano hayo, katika mahojiano na shirika hilo hilo la habari, walisema: "Takriban wafanyakazi 300 wa kitengo cha "akili mnemba" cha Google, wanaofanya kazi katika ofisi ya kampuni hiyo iliyoko London, wameshiriki katika maandamano hayo.
Kwa hakika, ushirikiano baina ya Israel na Google unafanyika chini ya makubaliano ambayo yalisainiwa hapo awali, na kwa mujibu wake, utawala wa Kizayuni unamiliki nafasi ya kuhifadhi data ya wingu yenye thamani ya dola bilioni 1.2 katika kampuni za Google na Amazon.
Maoni yako